Skip to main content

10H(ii)-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe12-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Ayafumbie Macho Baadhi Ya Makosa Ya Mkewe Madhali Si Yenye Kukiuka Maagizo Ya Allaah

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الزَّوَاجِ

Kitabu Cha Ndoa

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

Alhidaaya.com

11:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 8-Ayafumbie Macho Baadhi Ya Makosa Ya Mkewe Madhali Si Yenye Kukiuka Maagizo Ya Allaah:

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuongoza katika hili akituambia:

"لَا يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ"

“Muumini wa kiume (mume) asimbughudhikie Muumini mwanamke (mkewe).  Kama atachukizwa na baadhi ya tabia zake, basi zingine zitamfurahisha”.  [Swahiyh Muslim (1469)]