Skip to main content

10H(ii)-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe14-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Asimsuse Na Ikibidi Basi Yaishilie Ndani Ya Nyumba Tu

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الزَّوَاجِ

Kitabu Cha Ndoa

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

Alhidaaya.com

13:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe:  10-Asimsuse Na Ikibidi Basi Yaishilie Ndani Ya Nyumba Tu:

Ni kama ilivyoeleza Hadiyth iliyotangulia nyuma:

"وَلَا تَضْرِبِ اَلْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ، ولا تَهْجُرْ إِلا في البَيْتِ"

“Wala usipige uso, wala usimkashifu (kumwambia) ni mbaya, wala usimhame isipokuwa ndani ya nyumba tu”.  [Hadiyth Hasan.  Imechakatwa na Abu Daawuwd (2142), Ibn Maajah (1850), Ahmad (4/447) na An-Nasaaiy katika (Al-‘Ishrah) (269)]

Lakini kama kuna maslaha ya kisharia ya kumhama na kumsusa nje ya nyumba, basi atafanya hivyo kama alivyowahama Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakeze nje ya nyumba zao kwa muda wa mwezi mzima.