21-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Haki Za Pamoja Kati Ya Mke Na Mume
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
20: Haki Za Pamoja Kati Ya Mke Na Mume:
1- Kustarehe kila mmoja na mwenzake:
Hili linafanyika baada ya ‘aqdi kufungwa na masharti yakatimia ikiwa ni pamoja na mke kukabidhiwa kwa mumewe, kupatiwa mahala pa kukaa na kupatiwa matumizi. Kadhalika, kukosekana vizuizi kama kuhirimia na kadhalika. Yakitimu haya, basi kila mmoja ana haki ya kustarehe na mwenzake kwa mujibu wa maelekezo ya kisharia yaliyoelezewa nyuma.
2- Kurithiana:
Baada tu ya kufungwa ‘aqdi, basi haki ya kurithiana inathibiti kati yao akifa mmoja wao.
3- Kutangamana na kuamiliana kwa wema kama ilivyobainishwa nyuma.
4- Uharamu wa ukwe unathibiti kama ilivyobainishwa kwenye mlango wa wanawake walioharamishwa kwa sababu ya ukwe.
