01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa:Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa: Anayezalisha Na Kuwapa Watu Habari Ya Kuzaliwa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ

 

Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa:

 

Alhidaaya.com

 

 

 

01:  Anayezalisha Na Kuwapa Watu Habari Ya Kuzaliwa:

 

 

Mwanamke mwenye utaalamu wa kuzalisha, ndiye anayetakiwa kusimamia shughuli ya kumzalisha mwanamke mwenzake.  Awe na wanawake wenzake watakaomsaidia kufanikisha zoezi hilo.  Kazi hii kufanywa na wanawake ni jambo la waajib, ila tu kama kuna udharura usioepukika, kama kutopatikana wanawake wenye utaalamu wa kazi hii.  Wasipopatikana, basi daktari mwanaume wa Kiislamu atasimamia jukumu, lakini kwa kuchunga vidhibiti vilivyotajwa kwenye mlango wa Hukumu Za Kuangalia.

 

Inapendeza Kuwapa Watu Habari Ya Furaha Ya Kuzaliwa Mtoto Na Kuwapongeza Wahusika:

 

Mara mtoto anapozaliwa akatoa sauti ya kilio, imesuniwa kwa mwanamke aliyepo kwenye tukio, au yeyote aliye karibu, atoe habari ya furaha kwa baba yake, kwani hilo bila shaka linaingiza furaha moyoni.  Imesuniwa Muislamu kuharakia kumfurahisha nduguye na kumjulisha jambo lolote la kumfurahisha.

 

Allaah Ta’aalaa Akizungumzia kisa cha Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) Anasema:

 

"فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ"

 

 

Basi Tukambashiria ghulamu mvumilivu”.  [As-Swaaffaat: 101]

 

Na Anasema tena:

 

"قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ"

 

(Malaika) wakasema:  Usiogope!  Hakika sisi tunakubashiria ghulamu mjuzi”.  [Al-Hijr: 53]

 

Vile vile Anasema:

 

"يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا"

 

(Akaambiwa):  Ee Zakariyyaa!  Hakika Sisi Tunakubashiria ghulamu jina lake Yahyaa, Hatukupata kabla kumpa jina hilo yeyote.   [Maryam:  07]

 

Ikiwa mtu atapitwa na habari hiyo ya furaha, basi imesuniwa ampongeze mzazi kwa kukiombea kichanga chake kheri.

 

 

Share