Khomeini Ndani Ya Darubini - 1: Fatwa Za Wanazuoni Wa Kiislamu Kuhusiana Na Khomeini

 

Khomeini Ndani Ya Darubini – 1

Fatwa Za Wanazuoni Wa Kiislamu Kuhusiana Na Khomeini

 

Imeandikwa na Wajiyh Al-Madini

 

Toleo la Pili

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Yaliyomo

 

 

Utangulizi

 

 1. Kwanini Wanazuoni wa Kiislamu wamemhukumu Khomeini?
 2. Hoja zake kwamba MaImaam wa Kishia ni bora kuliko Malaika wote na Rusuli.
 3. Hoja yake kwamba mafundisho ya Imaam ni sawa na Qur-aan.
 4. Khomeini na kumvunjia heshima Rasuli wa Allaah.
 5. Dai la Khomeini kwamba Wahyi haukusita kushuka baada ya kifo cha Rasuli.
 6. Kuwashutumu Swahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
 7. Kikao cha Khomeini na kundi lake kuhusiana na Rasuli Mtukufu.
 8. Ulezi wa Mwanasheria “Wilaayatul Faqiyh”.
 9. Neno la muhtasari.
 10. Namna ya imani ya “Ulezi wa Mwanasheria - Wilaayatul Faqiyh” ulivyoingia kwenye mawazo ya Mashia.
 11. “Ulezi wa Mwanasheria - Wilaayatul Faqiyh” nini maana yake?
 12. Hitimisho

 

 

 

Muhtasari

 

Shukrani zake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ambaye shukurani zake zinajitosheleza, amani iwe juu ya watumwa wake teule.

 

Ulimwengu wa Kiislamu, umekutana na madhara makubwa katika wakati wa historia, kutoka kwa Mapinduzi ya Mashia wa Iran. Mapinduzi haya yana lengo lenye kudidimiza imani ya Waislamu na unajaribu kuubadilisha kwa kurudisha imani za kishirikina ziliopo kabla ya Uislamu, kuushinda na kuuangusha Ulimwengu wa Kiislamu na kuuharibu kwa kushirikiana na maadui wa Allaah: Makomonisti, Mayahudi, madhehebu ya siri, Mazindiq, na wasioamini Mungu.

 

Kwa vile vijana wa Kiislamu hawaelewi akili na dhamira ya Khomeini, viongozi wa Mapinduzi haya na pia hawayatambui malengo anayoyatafuta, giza la hatari linalisubiri Ulimwengu wa Kiislamu kama wataendelea kukumbatia kwa maneno matamu ya upotovu yanayotolewa na baadhi ya viongozi wakuu ndani ya Mapinduzi.

 

Tunapenda kuripuwa katika hotuba hii fupi upande mmoja wa nia sahihi ya kiongozi wa Mapinduzi ya Iran, na kukanusha uwongo wa maneno aliyotowa kwenye hafla mbalimbali. Kwa wakati huu, tutabainisha ushahidi wa sheria ambao fatwa umeziegemeza kumlaumu Khomeini kwa ukafiri na kumkufuru Mungu na upotevu, zilizotolewa na wanazuoni wa kuaminiwa kutoka kila pembe ya ulimwengu wa Kiislamu.

 

Hotuba hii inalenga kutumika kama indhari kwa wale wazembe miongoni mwa Waislamu, na pia kujitoa lawama juu yetu kwa Allaah, Bwana wa Ulimwengu, na (kutoa) ushauri mweupe kwa Ummah. Hakika Allaah Anailinda dini yake na ujumbe kutokana na wasioamini Allaah.

 

..ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ﴿٣٠﴾

Na wanapanga makri, na Allaah Anapanga makri (kupindua njama zao), na Allaah ni Mbora wa wenye kupanga makri. [Al-Anfaal:30]

 

- Mwandishi

 

 

Maneno Ya Mchapishaji

 

Shukrani zote ni za Allaah ambaye hutoa, kumpandisha na kumshusha hadhi yeyote ampendaye. Naye ni Mbora wa Uadilifu na Mwenye Enzi. Amani zimshukie juu ya Muhammad, Rasuli wa Rehma kwa ulimwengu, nuru ya viumbe wote na mbora wa Mitume yote ya Mungu.

 

Answaar wa Jumuiya ya Imaam ‘Aliy ina furaha kuwatambulisha wasomaji wetu hotuba hii yenye fikra: “Fatwa Za Wanazuoni Wa Kiislamu Kuhusiana Na Khomeini”ili kuweka bayana uongo wa tuhuma alizotoa Khomeini na mengi ya maneno ya kumtukana Mungu ambazo zimesababisha mgawanyiko wa kutoridhiana miongoni mwa daraja za taifa la Kiislamu.

 

 

Khomeini anadai yeye kuwa ni muaminifu na mfuasi mzuri wa Imaam ‘Aliy na watu wake wa nyumbani, lakini ukweli unaonesha vengine. Hakika, Khomeini ni adui mkuu wa Imaam ‘Aliy kwa sababu zifuatazo:

 

 

Kwanza, Imaam ameridhia maswahaba watatu wa Rasuli Muhammad, kwa kuwapa ushauri mzuri, na kuwatumikia kama ni askari muadilifu na mshauri anayeaminiwa. Hakupata kuwatukana wala kuwatoa makosa (yasiyo na msingi) seuze kuwanasibisha kwa kumtukana Allaah au kuwakana. Lakini Khomeini anayedai kuwa ni mfuasi wa ‘Aliy amemtukana Abu Bakr na ‘Umar, kuwatuhumu wao na Ummah mzima wa Rasuli kwa kumkufuru Allaah, hivyo kwenda kinyume na Imaam ‘Aliy na kujitukana yeye mwenyewe pale ambapo amewatuhumu Maswahaba kwa kufru.

 

 

Pili, amemtuhumu Imaam ‘Aliy na Imaam wa Kishia kwa kushindwa kusimaamisha haki na mambo mema. Amejifanya yeye na Imaam wake waliofichikana kuwa ndio wenye vigezo vya kuwa viongozi wa kusimaamisha haki na mambo mema, hivyo kumshusha hadhi Imaam ‘Aliy na jitihada zote za Rasuli na Swahaba wake na Maimaam.

 

 

Tatu, Khomeini anarudia uongo wa kizindiyq kama wa Yahudi Abdullah Ibn Sabaa (na) wafuataji wake ambaye anadai kwamba Imaam ‘Aliy alikuwa ni njia ya wahyi kwa Rasuli, kwamba alikamata elimu yote ya Uislamu na siri zote za dini ya Kiislamu, kwamba yeye ndiye mtukufu wa Rusuli wa Allaah. (Ukweli ni kuwa) Imaam ‘Aliy aliwapiga vita watu wa Masabaiya (wafuasi wa Abdullah bin Sabaa Myahudi), kuwatafuta kwenye kila mji na kijiji, kwamba alimpiga vita kiongozi wao Abdullah Ibn Sabaa kwa kumuua.

 

 

Naapa kwa Allaah, yareti Imaam ‘Aliy ni yuhai na anaongoza, kitu cha mwanzo angelikifanya ni kummaliza Khomeini na jeshi lake la askari ambao wamekwenda kinyume na Dini ya Allaah na kumnasibisha ‘Aliy yale ambayo Mazindiyq wa Abdullah bin Sabaa walivyomdai kuwa navyo. Hakika Khomeini na wafuasi wake wanadai kwamba mke mwema wa ‘Aliy, mama wa wanawake Peponi amesema: “Nimepokea wahyi baada ya kifo cha Rasuli. Kwa siku sabiini na tano Malaika Jibril akinitembelea, akinisomea Qur-aan iliyo kubwa mara tatu zaidi kuliko ile iliyoteremshwa kwa baba yangu. Haina hata herufi moja kutoka kwa Qur-aan ya baba yangu”. Hivyo, hao Mazindiyq wamemhukumu Faatwimah, Allaah awe Radhwi naye, kwa kufru, na kujitangazia wahyi juu yake, kwa kusema Qur-aan ilikuwa sio ya kweli na kwa kumuelezea uwongo Rasuli.

 

 

Kwa yote hayo, Answaar wa Jumuiya ya Imaam ‘Aliy umeona haja kuitetea Dini ya ‘Aliy, heshima na imani. Hakuna utetezi bora kuliko kusimama dhidi ya adui zake ambao wanawaghilibu Mashia kwa jina lake na kupenyeza uzushi ulio mzito wa dhalimu juu ya jamii ya Kishia.

 

 

Matokeo yake, Khomeini na wanaomfuata ni maadui wakuu wa Imaam ‘Aliy na watoto wake wema, kwani wao wamewasifia hao Maimaam kwa kuwapachika alama za Uungu, kama kumiliki elimu ya nyanja zote hata kuongoza nukta (atoms) za Ulimwengu. Waongo hao wamedai kwamba Imaam wa Kishia wamejipa nguvu hizi wao wenyewe, kuwatukana Swahaba wa Rasuli, kudai kufru kwa Waislamu, kudai kwamba Qur-aan haikukamilika na hata kuharibiwa, wamesema kwamba wamepokea wahyi na kwamba wameumbwa kutokana na nuru ya Allaah, na kwamba wanaweza kumuingiza Peponi yeyote wampendae, na kumtoa Motoni yeyote wampendae. Walidai kuwa watawaua wote wanaopingana na wao, kuwaharibu Waislamu wote na kulipiza kisasi juu ya Abu Bakr na ‘Umar kwa sababu wao walitoa hoja na kumnyang’anya haki zake na kumzuia urithi, utaifa wao na milki yao. Lakini madai yote haya ni uongo uliotolewa kwa Imaam ambao walikuwa ni mfano wa maadili mema, hekima, elimu na imani.

 

 

Kwa tuhuma na uongo wote hapo juu, wafuataji sahihi wa Imaam ‘Aliy wanalazimika kuwapinga hao waongo na kuripua tuhuma zao na uongo wao kwa kila mtu ili kulinda heshima ya Imaam ‘Aliy, jemedari wa imani, na zile tuhuma dhidi ya watoto wake wema kuilinda imani ya Waislamu kutokana na wartadi wa kizindiq.

 

Hivyo, tunamuomba Mola Mtukufu kuikubali kazi hii kwa ajili yake pekee.

 

I Kwa Nini Wanazuoni Wa Kiislamu Wamemuhukumu Khomeini Kwa Kufru?

 

Jumuiya tofauti za Kiislamu zimetoa tamko la uoni wa kishari'ah kutokana na kufru na kurtadi kwa Khomeini. Jumuiya zinajumuisha Ushirika wa Waislamu Duniani (Muslim World League) ambao ulitoa fatwa kwa kadhia hiyo tarehe 9 ya Ramadhaan mwaka 1400 H. (1980), na nyengine katika mkutano wa tatu wa kila mwaka Swafar 1408/1987; Wizara ya Mali na Masuala ya Dini ya Morocco, 1400 H, ash-Shaykh al Habib Bal-Khojah, mshauri wa sheria Jamhuri ya Tunisia, fadhilah ash-Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz bin Baaz, ash-Shaykh Naaswirud-Diyn al-Albaaniy ambaye ni bingwa wa Fiqhi ya Sunnah ya Rasuli na wanazuoni wengi wengineo kwenye ulimwengu wa Kiislamu.

 

 

Kwa vile wanafunzi wengi wa elimu, na pia jamii ya kawaida, wanawezekana kuwa hawaelewi ushahidi wa kishari'ah juu ya marejeo ya hukumu ya kishari'ah, wengine inawezekana hata wakawaza kwanini Khomeini alihukumiwa kwa Kufru. Kwa sababu hii, tunapendelea kunakili katika hotuba hii matamko na maoni yaliyotolewa naye, na kufuatana nazo kwa hoja za kishari'ah ambazo zinaripua asili ya kufru. Hii itafanya kama ni kutoa ushahidi dhidi ya makafiri na waasi, na pia juu yetu kujitoa kwenye lawama mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

قَالُوا مَعْذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٦٤﴾

Tupate kuwa na udhuru mbele ya Rabb wenu na huenda wakawa na taqwa. [Al-A’raaf: 164]

 

…/2

 

 

Share