Suwrah Gani Za Kusoma Siku Ya Ijumaa?

 

SWALI:

 

asalama alaiekum insh this mail will find you ok.i have masuala kidogo naomba mnipatie majibu.

...moja.....nimewahi kusikia kuwa siku ya ijumaa ktk sala ya alfajiri, ni sunna  rakaa ya mwanzo kusoma suratul sajdah na rakaa ya pili kusoma suratul dahr,well jee kuna ushahidi wa hayo ktk hadithi etc?

...mbili.....nimeshaona watu wengi kila siku ya ijumaa mtu anakuwa anadumu kw kusoma suratul kahf,jee kuna ushahidi ktk kuran au hadithi,na kuna faida gani kusomwa hiyo sura?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kuhusu Surah za kusomwa katika Swalah ya Alfajiri ya Ijumaa ni swahiyhi kwamba ni Sunnah kusoma Suratus-Sajdah katika Rakaa ya mwanzo na Suratul-Insaan (Au Suratud-Dahr) katika rakaa ya pili. Dalili imethibiti katika usimulizi mbali mbali, mmojawapo ni Hadiyth ifuatayo:

 

  عن ابن عباس :  أن النبي صلى الله عليه وسلم كان يقرأ في صلاة الفجر يوم الجمعة : ((الم تَنْزِيلُ الْكِتَابِ)) السجدة ، و ((هَلْ أَتَى عَلَى الْإِنْسَانِ حِينٌ مِنَ الدَّهْرِ ) ) رواه مسلم

Kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma siku ya Ijumaa katika Swalah ya Alfajiri ((Alif Laam Tanziylul-Kitaabi)) [As-Sajdah] na ((Hal Ataa 'alal-Insaani Hiynum-minad-Dahr)) [Al-Insaan] [Muslim]

 

Akisoma Surah hizi na kuziacha mara nyingine kwa kusoma nyingine ili kutuonyesha kwamba sio lazima zishikiliwe Surah hizi pekee Swalah ya Alfajiri Ijumaa, bali inawezekana kubadilisha.

 

Ufahamu usio sahihi kwa baadhi ya watu ni kwamba Surah hii ameisoma Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya Sajdah iliyokuwemo hivyo huiita Sajda ya Ijumaa, kwa hiyo hudhani kwamba lazima ipatikane Surah yenye sajdah ikiwa haikusomwa Surah hii. Bali iliyokusudiwa ni maana zilizokuwemo katika hizi Surah tukufu kama alivyosema Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah kwamba Surah hizi mbili zinalingana katika kutajwa maumbile ya binaadamu, kutajwa siku ya kufufuliwa viumbe ambayo ni siku ya Ijumaa hivyo kusomwa hizi Surah ni ukumbusho kwa ujumla yaliyomo.

 

Makosa mengine ni baadhi ya watu kusoma Surah mojawapo ya hizi mbili kwa kuzigawa nusu yaani kusoma nusu yake katika rakaa ya mwanzo na kumalizia nusu yake katika rakaa ya pili. Inatakiwa kufuatwa kama ilivyokuja mafunzo katika Sunnah kwa kuzisoma zote mbili, rakaa ya kwanza Suratus-Sajdah kamili, na rakaa ya pili Suratul-Insaan kamili.   

 

Kuhusu kusomwa Suratul Kahf siku ya Ijumaa nayo pia imethibiti katika dalili kwamba inapaswa kusomwa kutokana na fadhila zake zifutazo:

(( قال عليه الصلاة والسلام : من قرأ سورة الكهف ليلة الجمعة، أضاء له من النور ما بينه وبين البيت العتيق) )  صححه الألباني في صحيح الترغيب والترهيب  

((Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم   Atakayesoma Suratul-Kahf usiku wa Ijumaa, ataangaziwa na nuru baina yake na baina ya nyumba kongwe (Al-Ka’abah)) [Swahiyh katika Silsilatul-Ahaadiyth As-Swahiyhah cha Shaykh Al-Albaaniy]

Pamoja na kusemwa kuwa Hadiyth hiyo imetoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم, lakini Wanachuoni wa Hadiyth wengi wamesema ni Hadiyth 'Mawquuf' ambayo haijaelezwa na Mtume bali ni kutoka kwa Maswahaba, na kwa nyongeza ya neno 'atakayeisoma Ijumaa' haikuthibiti kwa Mtume, na maelezo hayo hapo juu ni ya kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy na yeye ndiye aliyekuwa akiisoma Surah hiyo katika siku ya Ijumaa, na Wanachuoni wanasema kuwa maadam Maswahaba walikuwa wakiisoma Surah hiyo siku ya Ijumaa, basi hakuna neno kuisoma Ijumaa, japo kuisoma siku yoyote ni sawa na mtu atapata fadhila zilizotajwa kwenye Hadiyth hiyo. Ama kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم, Wanachuoni wamesema haikuja na lafdhi ya 'kuisoma Ijumaa', bali imekuja kwa ujumla wake wa kuisoma Surah hiyo siku yoyote ile kama ilivyokuja hapa chini:

 

((وقال صلى الله عليه وسلم : من قرأ سورة الكهف كما أنزلت كانت له نورا يوم القيامة ، من مقامه إلى مكة ، و من قرأ عشر آيات من آخرها ثم خرج الدجال لم يضره ....))  صححه الألباني في سلسلة الأحاديث الصحيح 

((Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم atakayesoma Suratul-Kahf kama ilivyoteremshwa, atakuwa na mwangaza siku ya Qiyaamah pale alipo mpaka Makkah, na atakayesoma Aayah kumi za mwisho kisha akitokea Dajjaal hatomdhuru)) [Swahiyh kama alivyoeleza Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilatul-Ahaadiyth As-Swahiyhah]

 

Na Allaah Anajua zaidi

  

Share