14-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kutayamamu Badala Ya Wudhuu Katika Hali Ya Janaba

 

 

Vile vile inaruhusiwa kufanya Tayammum mara nyingine badala ya wudhuu kabla ya kulala. Hii ni kutokana na Hadiyth ya Bibi ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye amesema:

 

كانَ رسولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلّم إذا أجنبَ فأرادَ أنْ  ينامَ توضأَ

 

"Mtume alipokuwa katika hali ya janaba na kila alipotaka kwenda kulala alikuwa akichukua wudhuu au akitayammum".[1]

 

[1] Al-Bayhaaqiy na Ibn Abi Shaybah: Hasan

Share