Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri

Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri

 

Vipimo vya Wali:

Mchele basmati - 3 magi (kikombe kikubwa)

Mchanganyiko wa mboga za barafu

(Frozen vegetables) - 1 ½ mug

Chumvi - kiasi

Mafuta - 3 vijiko vya chakula

Kitungu maji (kilichokatwa) - 1

Bizari ya pilau (nzima) - 1 kijiko cha chakula

 

Namna Ya kutayarisha na kupika:

 1. Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
 2. Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 6.
 3. Tia chumvi.
 4. Yakisha kuchemka unatia mchele, chemsha usiive sana, uive nusu kiini. Mwaga maji na kuchuja wali.
 5. Unamimina Yale mafuta kwenye sufuria unakaanga bizari ya pilau kidogo na kitunguu kabla ya kugeuka rangi ya hudhurungi (brown).
 6. Tia mchanganyiko wa mboga za barafu.,  
 7. Mimina wali, changanya vizuri, ufunike na uweke katika moto mdogo kwa dakika 20.
 8. Pakua tayari kwa kuliwa.

 

Vipimo Vya Mchuzi 

Kuku - 2 Ratili (LB)

Chumvi - Kiasi

Mafuta - ¼ Kikombe

Nyanya Kata vipande - 4

Nyanya kopo - 2 vijiko wa chakula

Tangawizi - 1 kijiko ya chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko ya chakula

Tanduri masala - 1 kijiko cha chakula

Kotmiri liliyokatwa - 3 vijiko vya chakula

Pilipili mbichi - 2

Pili masala - 1 kijiko cha chakula

Garam masala - ½ kijiko cha chakula

Bizari manjano - ½ kijiko cha chakula

Mtindi - 3 vijiko vya chakula

Pilipili boga (kata vipande virefu) - 1

Ndimu - 2 vijiko vya chakula

 

Namna ya kutayarisha na kupika:

 1. Kwenye bakuli tia kuku na changanya vitu vyote pamoja isipokua mafuta.
 2. Tia mafuta kwenye sufuria yakisha kupata moto mimina kuku  umpike kwa muda ½ saa kwa moto kiasi.
 3. Pakua kuku kwenye bakuli au sahani na ukate vitunguu maji duara na umpambie. Tayari kwa kuliwa.

 

Share