Kuku Wa Sosi Ya Ukwaju Wa Kuchomwa Katika Mkaa Na Saladi Ya Orzo

Kuku Wa Sosi Ya Ukwaju Wa Kuchomwa Katika Mkaa  Na Saladi Ya Orzo  

  

Vipimo 

Kuku (miguu na paja) Safisha, osha kwa chumvi na siki atoke harufu - 12 mapande

Tangawizi mbichi iliokatwakatwa - 1 kipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) Menya- 1 uwa zima

Pilipilimbichi - 6

Pilipili mbuzi - 3

Ukwaju iliprowekwa na kukamuliwa - 1 kikombe cha chai

Bizari ya pilau/jiyra/cumin - 1 kijiko cha chai

Bizari ya gilgilan/Dania/coriander - 1 kijiko cha chai

Bizari ya manjano/haldi/tumeric - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 2

Namna Ya Kupika:   

  1. Chanachana  (slit) mapaja ya kuku kwa ajili ya kuingiza masala.  
  2. Katika mashine la kusagia (blender) weka tangawizi mbichi, kitunguu thomu, pilipili mbichi na mbuzi, bizari zote, chumvi na ndimu. 
  3. Saga hadi ilainike.  
  4. Weka kuku katika bakuli umimine mchanganyiko wa masala. Changanya vizuri kuku aingie masala kila mahahli. 
  5. Roweka (marinate) kwa muda wa masaa mawili au zaidi, huku unageuzageuza akolee pande zote.    
  6. Choma katika mkaa hadi aive. 
  7. Epua kulia na saladi ya orzo   

Upishi wa saladi ya Orzo unapatikana katika kiungo kifuatacho: 

Saladi Ya Orzo Ya Kigiriki (Greek Orzo Salad)   

Kidokezo:   

Unaweza kuroweka tokea usiku ukaweka katika friji, ikiwa unataka kipimo kingi kwa kuongezea vipimo vya masala.

 

 

 

 

 

Share