Kupaka Dawa Ya Maumivu Ya Kichwa Inabatilisha Swawm?

 SWALI:

 

 

 

Assalam Alykhum wa Rahmantul Lahi wa Barakatu

 

Swali langu je inafaa kupaka vicks kwenye kichwa ukiwa umefunga?

 

Jazzaka  Allah elf Kheri

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

 

Dawa za kupaka mwilini  kwa ajili ya maumivu ikiwa ni kwa ajili ya kichwa au maumivu sehemu nyinginezo hazibatilishi Swawm. Hivyo unaweza kupaka  vicks na Swawm yako sahihi.

 

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo kuhusu mambo yanayobatilisha Swawm na yasiyobatilisha.

 

 

Mambo Muhimu Kuhusu Swawm

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share