Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

   

Vipimo

Muhogo - 3                                             

Tui La Nazi - 2 vikombe

Chumvi - kiasi

Pilipili mbichi - 2

Mafuta - 1 kijiko moja

Kitunguu maji - 1 kidogo

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
  2. Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
  3. Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
  4. Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine.

 

 

 

 

 

 

Share