Wali Wa Nazi Wa Adesi, Bamia Na Mchuzi Wa Kamba

Wali Wa Nazi Wa Adesi, Bamia Na Mchuzi Wa Kamba

Vipimo 

Mchele - 2 vikombe

Adesi -1 ½ vikombe

Nazi ya unga - 1  Kikombe

Maji (inategemea mchele) - 3

Chumvi - Kiasi

 

 

Vipimo Vya Bamia:

Bamia - ½ kilo 

Vitunguu maji - 2 vya kiasi

Nyanya iliyosagwa - 1 kubwa                                                                             

Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya chai

Pilipili manga - ½ kijiko cha chai

Mafuta - 3 vijiko vya chai

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Wali wa adesi

  1. Osha na roweka mchele na adesi .
  2. Chuja nazi kwa vikombe 3 vya maji tia chumvi kisha weka jikoni.
  3. Tui la nazi likishachemka tia mchele na adesi pamoja.  Punguza moto, funika wali upikike   kwa moto mdogo mpaka ukauke vizuri.

 

 

Bamia

  1. Katakata bamia vipande  vya kiasi/ Katakakata vitunguu weka kando.
  2. Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi.
  3. Tia nyanya  ilosagwa na nyanya ya kopo na pilipili manga na chumvi.
  4. Kisha Tia bamia punguza moto mdogo mdogo mpaka ziwive.

Vipimo: Mchuzi Wa Kamba

Kamba - 1Lb

Vitunguu  vilokatwa katwa - 2

Nyanya   ilokatwa katwa - 2

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 Kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi  (curry powder) - ½ Kijiko cha chai

Haldi – bizari ya manajano - ½  kijiko cha chai

Nyanya ya kopo - ½ Kijiko cha chai

Ndimu - 1

Chumvi - Kiasi

Mafuta ya kukaangia - 2 Vijiko vya supu

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kaanga vitunguu kidogo hadi vilainike,
  2. Tia nyanya, thomu na piilipili mbichi.  Endelea kukaanga, tia nyanya ya kopo, chumvi, bizari zote.
  3. Tia tia kamba na huku unakoroga mpaka wabadilike rangi na kuwiva. Kamulia ndimu na mchuzi uko tayari..

 

 

 

 

 

 

Share