05-Fatwa: Kuwakilisha Katika Kulipa Zakaatul-Fitwr

 

Kuwakilisha Katika Kulipa Zakaatul-Fitwr

 

 www.alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Baadhi ya miskiti wanaashiria kupokea kiwango cha Zakaatul-Fitwr kutoka kwa watu ili wagawe kwa wanaohitaji kwa ajili yao. Hugawa  chakula kama mchele, unga n.k. Je, desturi hii ni sawa?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah

 

Kwa vile imekusudiwa kununua na kugawa bidhaa  kwa wanaohitaji (hizo bidhaa) kwa ajili yao, hivya ni sawa na watapa thawabu In Shaa Allaah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share