14-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Zakaatul-Fitwr Kwa Aliyefariki Kabla Au Baada Ya Magharibi Siku Ya Mwisho Ramadhwaan

Zakaatul-Fitwr Kwa Aliyefariki Kabla Au Baada Ya Magharibi Siku Ya Mwisho Ramadhwaan

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI: 

 

Nini hukmu ya mtu aliyefariki kabla ya Magharibi na mwengine baada ya Magharibi siku ya mwisho ya Ramadhwaan?

 

JIBU:

 

Zakaatul-Fitwr si waajib kwa yeyote aliyefariki kabla ya Magharibi siku inayofuatia ‘Iydul-Fitwr  kwa sababu inawajibika baada ya Magharibi tu ya usiku wa mwisho wa Ramadhwan na aliyetajwa wa kwanza katika swali amefariki kabla ya Magharibi. Ama aliyefariki baada ya Magharibi imewajibika kwake Zakaatul Fitwr kwa sababu amefariki baada ya wakati uliowekewa shariy’ah Zakaatul-Fitwr kuwajibika.

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah  (20514)]

 

 

 

 

 

 

Share