31-Fatwa: Ni Kweli Swawm Inanin'ginia Baina Ya Mbingu na Ardhi Hadi Mtu Atoe Zakaatul-Fitwr?

Ni Kweli Swawm Inanin'ginia Baina Ya Mbingu na Ardhi Hadi Mtu Atoe Zakaatul-Fitwr?

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

Je, Hadiyth inayosema kuwa Swawm ya Ramadhaan inaning'inia baina ya mbinu na ardhi na haipandishwi juu hadi ilipwe Zakaatul-Fitwr ni Sahihi? 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hadiyth hiyo ni dhaifu.

 

Katika Al-Jaami' as-Swaghiyr, as-Suyuwtwiy ameihusisha kwa Ibn Shaahiyn katika Targhiyb yake: "Imesimuliwa katika Adhw-Dhwiyaa' kutoka kwa Jariyr bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: Mwezi wa Ramadhaan unaning'inia baina ya mbingu na ardhi na (Swawm) haipelekwi juu kwa Allaah isipokuwa kwa (kutolewa) Zakaatul-Fitwr"

 

Imechambuliwa kuwa ni dhaifu na as-Suyuwtwiy. Al-Manaawiy ameeleza sababu yake katika Faydhw Al-Qadiyr ambako amesema: "Imesimuliwa na Ibn Al-Jawziy katika Al-Waahiyaat na kasema: Sio Swahiyh, isnaad yake inajumuisha Muhammad bin 'Ubayd al-Baswriy ambaye ni majhuwl (asiyejulikana).

 

Imechambuliwa pia kuwa ni dhaifu na Imaam al-Albaaniy katika as-Silsilatul-Ahaadiyth ad-Dhwa'iyfah (43). Kasema: "Hata kama ingekuwa ni Hadiyth Swahiyh, basi maana iliyodhihiri ni kukubaliwa kwa Swawm ya Ramadhwaan inategemea baada ya kulipa Zakaatul-Fitwr tu, na ikiwa mtu hakulipa, basi Swawm  yake haitokubaliwa. Lakini simjui Mwanachuoni yeyote aliyesema hivyo na Hadiyth sio Swahiyh" [mwisho wa kunukuu]

 

Kwa vile Hadiyth sio Swahiyh, hakuna atakayeweza kusema kwamba Swawm ya Ramadhwaan inakubalika tu baada ya kutoa Zakaatul-Fitwr kwa saabu hakuna atakayejua hivyo isipokuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Imethibitika katika Sunan Abi Daawuwd kwamba Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kuwalisha masikini kama ni kutakasa swiyaam za aliyefunga kutokana na maneno ya upuuzi na kauli chafu" [Imepewa daraja ya Hasan na Shaykh al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan Abi Daawuwd] 

 

Hadiyth hii inaelezea hikma ya Zakaatul-Fitwr ambayo kufidia kasoro yoyote iliyotokea katika Swawm. Haisemi kuwa Swawm haitokubaliwa ila tu baada ya kutoa Zakaatul-Fitwr.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share