Mkate Wa Tambi Za Kuoka

Mkate Wa Tambi Wa Kuoka

 

Vipimo:

Tambi Za Mchele -  1 Pakti  (400 mg)

Tui la nazi -  1 Kikombe

Sukari - 1/2 kikombe  

Maziwa ya chai ya kopo (evaporated milk) -  1/2 kikombe

Samli - 1 kijiko cha supu

Zabibu - 1/4 kikombe

Hiliki - 1/4 kijiko cha chai

Arki (rose flavour) -  Matone machache 

Namna ya Kutayarisha na Kupika

  1. Katakata tambi kisha zichemshe kidogo tu katika maji  yanayochemka na uzichuje  (zisiwive sana)
  2. Chemsha tui la nazi, pamoja na vitu vyote vingine, koroga  vichanganyike  katika moto.
  3. Tia tambi na koroga vizuri ziache katika moto zipikike na kuwiva.
  4. Paka samli kikaango cha kupikia kilichokuwa kina shimo zaidi (deep frying pan) kisichokuwa na mkono au tumia treya ya keki iliyo nzito kidogo.
  5. Zinapokaribia tambi kukauka mimina katika kikaango au treya ya keki.  
  6. Didimiza kwa mwiko kuzisawazisha zijifunge katika duara.
  7. Paka samli kidogo juu yake.
  8. Choma (bake katika oven) moto wa kiasi 350º kwa muda dakika 20 au hadi zikakauke na zianze kubadilika rangi.
  9. Zima moto wa chini kisha asha moto wa juu kidogo tu zipate kuleta rangi ya hudhurungi (brown) kama kwenye picha.
  10. Epua, na zitoe katika kikaango na uziweke katika sahani ya kupakuliwa. Tambi zitatokea kama mkate. Utakatakata vipande.

 

 

Share