Roti- Chapatti Za Trinidad Na Guyana

Roti- Chapatti Za Trinidad Na Guyana 

   

Vipimo: 

Unga mweupe - 6 Vikombe

Baking powder - 1 Kijiko cha supu

Samli au mafuta - 2 Vijiko vya supu 

Maji - 2 ¼    vikombe *

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia unga katika bakuli uchanganye pamoja na vitu vyote.
  2. Tia maji ya  dafudafu (warm) uchanganye unga vizuri, usikande kama zinavyokandwa chapatti, changanya tu vizuri sana. Tazama picha. *Unaweza kuongeza au kupunguza maji kutegemea unga wenyewe. Kiasi chake cha mchanganyiko kiwe kama unga wa chapatti.
  3. Funika unga katika bakuli lake, vizuri kwa karatasi ya plastiki usiingie hewa. Uache kwa muda wa nusu saa au zaidi kidogo. 
  4. Rudia kuuchanganya kisha fanya madonge.

        

  1. Sukuma donge upake mafuta kidogo sana kisha nyunyizia unga, na ukunjue kama ilivyo katika picha.

                          

  1. Ukimaliza madonge yote, weka kando na yaache tena kwa muda dakika kumi au robo saa.

                                          

  1. Pasha moto chuma. Sukuma donge la roti na upike roti kama kwenye picha. Usitie mafuta kama zinavyopikwa chapatti, bali pakaza mafuta kidogo sana kwa brashi (brush). Roti itafura wakati wa kuipika na kuiva vizuri ndani.

                                         

  1. Epua na hapo hapo roti ikiwa ingali imoto, ivunjevunje inyambuke, kisha unaweza kuikunja mkunjo  upendavyo kama ilivyo katika hizi picha hapa au kama ilivyo picha ya juu.

                                                              

  1. Roti ziko tayari kuliwa mchuzi au mboga yoyote.

Kidokezo:

Kawaida ya roti hizi hazitiwi chumvi, lakini ukipenda tia kidogo sana.

 

 

 

 

 

Share