Mume Kuoa Zaidi Ya Mke Mmoja Ikiwa Hana Nguvu Za Kuwatimizia Kitendo Cha Ndoa

 

SWALI:

assalam alaykum warahmatu llahi wabarakatu.

Naomba nijibiwe maswali yangu haya  Mungu awalipe kwa kutusaidia.

Kuowa mke zaidi ya mmoja ni snna katika uislam. je sunnah ni inaweza kurekelezeka ikiwa mwanamme hana nguvu za kutosha. nna maana kuwa hao wake wawili alonao hawatoshelezi katika suala la ndoa . kuna ulazima kufanya hivyo.

Naomba majibu wabillahi taufik.

Assalam alaykum


  

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Tumepokea maswali yako matatu ambayo umetuma katika barua moja, jambo ambalo tumesisitiza lisifanyike bali kila swali litumwe katika barua ya pekee. Kufanya hivi itakuwa wepesi kujibu kila swali na kulipa kila swali kichwa cha habari kinachostahiki na pia kupunguza usumbufu wa kuyagawa maswali. Hivyo tunakuomba wewe na ndugu wengine wote watekeleze haya muhimu wanapotuma maswali yao.

Ndoa katika Uislamu ni Sunnah iliyohimizwa sana kwa wafuasi wake waoe au waolewe, kwani katika Dini hii hakuna utawa. Kwa ajili hiyo pale Swahaba mmoja aliposema hatooa, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Yeyote mwenye kukengeuka na Sunnah yangu si katika mimi” (al-Bukhaariy na Muslim). Mbali na hilo ndoa inagawanyika sehemu kadhaa, miongoni mwazo ni:

(a)  Faradhi: Kwa yule mwenye uwezo wa pesa na hawezi kujizuilia ni lazima kwake aoe.

(b)  Haramu: Kwa yule ambaye hana uwezo wa kimwili wa kuweza kumkidhia mkewe kwa tendo la ndoa basi haifai kwake kuoa. Hilo ni kuondoa dhara kwa mwanamke.

Hizi ni baadhi ya vigawanyo vya ndoa. Hivyo, ikiwa mwanamme hana uwezo wa kutekeleza tendo la ndoa kwake itakuwa ni haramu kuongeza mke wa pili kwani dhara atakaloleta ni kubwa sana.

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share