Kumwita Mama Mdogo Au Mkubwa ‘Mama’ Inafaa?

 

SWALI:

Je inaswihi kwa mdogo wa kike wa mama yangu kumuita kwa jina la mama ni dhambi? Kwani wengi wetu tumezoea kuwaita wadogo zao mama zetu kwa jina la mama mdogo, au wakati mwengine kuwaita mama. 

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali. Hakuna tatizo lolote kwako au kwa Muislamu kumuita mama mdogo kwa jina la mama kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuambia: “Mama mdogo ni kama mama” (Abu Daawuud).

Hivyo, cheo chake ni kama cha mama na huwezi kabisa kumuoa daima kama vile mama kwa kauli yake Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala): “Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na halati (mama wadogo) zenu” ().

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share