Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Pilau Ya  Samaki Wa Tuna Na Mboga

 

Vipimo

Mchele  - 2 Mugs      

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg)  - Mug

Tuna (samaki/jodari) -  2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala - 1 kijiko cha supu

Nyanya - 2  

Kitungu maji -   1

Mdalasini nzima -  2 vijiti

Karafuu  - 6 chembe

Pilipili mbichi  - 1

Chumvi - kiasi

Viazi - 3

Maji - 2 ½ Mugs

Mafuta -  3 vijiko vya supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
  2. Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
  3. Mimina viazi, thomu na tangawizi,  bizari zote na kaanga.
  4. Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
  5. Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
  6. Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
  7.  Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari  kuliwa.

 

 

Share