Ijumaa: Khutba Ya Ijumaa Ikimpita Mtu Aswali Jamaa na Wengine?

 

SWALI:

Je swalla ya ijuma ni umuhimu kwa wanawake? Je, ukikuta khutba imekupita unaweza ukasali na wengine zile rakaa mbili tu?

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu aliyeuliza swali hili kuhusu Swalah ya Ijumaa. Hakika ya suala hilo ni kuwa wanawake hawajafaradhiwa kuswali Swalah ya Jama’ah ikiwa ni Ijumaa au nyinginezo. Hakika kwenda kwao Misikitini watapata faida nyingi kama kusikiliza mawaidha na khutbah za Ijumaa. Hata hivyo ni bora kwao kuswali nyumbani. Lakini ikiwa wanataka kuswali ndani ya Msikiti hawafai kukatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Musiwakataze vijakazi vya Allaah kwenda katika Misikiti ya Allaah” (al-Bukhaariy).

Ama kuhusu swali lako la pili ni kuwa, ukikosa Swalah ya Ijumaa pamoja na Imaam huwezi kuswali tena rakaa mbili bali itabidi hata ukiswali na jamaa kuswali Swalah ya Adhuhuri ambayo ni rakaa nne. Kwa maana itakuwa umeshaikosa Swalah ya Ijumaa. Hilo linafaa lituhimize sisi kwenda mapema siku ya Ijumaa ili tupate faida za khutba na kisha Swalah ya Ijumaa (rakaa mbili).

Na Allaah Anajua zaidi.

Share