Vipapatio Vya Kuku Vikalikali Na Tamu (Sweet and Sour Chicken wings)

Vipapatio Vya Kuku Vikalikali Na Tamu (Sweet and Sour Chicken wings)

 

Vipimo 

Vipapatio (Chicken wings) - 2LB

Chumvi - kiasi

Pilipilimanga - 1 kijiko cha chai 

Vitu vya Sosi 

Kitunguu saumu/thomu iliyosagwa - 2 vijiko vya supu            

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Paprika - 1 kijiko cha chai

HP sauce (ikiwa utapenda) - 2 vijiko vya supu

Ukwaju - 3 vijiko vya supu

Asali - 2 vijiko vya supu

Nyanya kopo - 1 kijiko cha chai

Tomato Ketchup - 2 vijiko vya supu

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Mafuta ya kukaangia vipapatio - kiasi katika karai  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Osha vizuri vipapatio kwa maji ya moto, chumvi na haldi (bizari ya manjano kukata harufu ya kuku.
  2. Tia vipapatio chumvi na pilipili kisha ukaange  katika mafuta mengi (deep fry) wakiiva na kubadilika rangi ya hudhurungi (golden brown) toa na uchuje mafuta.
  3. Katika karai nyingine, tia mafuta vijiko 2 vya supu, kisha anza  kukaanga thomu iliyosagwa kwa muda mdogo tu igeuke rangi kidogo.
  4. Tia vitu vyote vingine vya sosi uendelee kukaanga kidogo tu. Ikiwa sosi nzito ongeza ukwaju.
  5. Zima moto, changanya vipapatio vizuri na sosi, pakuwa katika sahani vikiwa tayari kuliwa.

 

 

 

 

Share