Fadhila Za Mwezi Wa Al-Muharram, Siku Ya 'Aashuraa Na Bid'ah Zake

 

Fadhila Za Mwezi Wa Al-Muharram, Siku Ya 'Aashuraa Na Bid'ah Zake

 

Alhidaaya.com

 

AlhamduliLLaah, Tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaaa) Kutufikisha tena katika mwaka mwengine mpya wa Kiislamu. Mwezi wa Al-Muharram una fadhila makhsusi kulingana na miezi mitukufu mingineyo. Moja wa fadhila hizo ni funga ya tarehe 9 na 10 Al-Muharram zinazojulikana kama Taasu'aa na 'Aashuraa. Hivyo ndugu Waislamu tusiache kufunga siku hizi mbili kwani thawabu zake ni kufutiwa madhambo ya mwaka mzima!

 

 قال النبي صلى الله عليه وسلم: ((صِيامُ يَوْمِ عَاشُورَاءَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ))  رواه مسلم

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swawm ya  siku ya 'Aashuraa, nataraji kutoka kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka uliotangulia)) [Muslim]

 

Bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Ukumbusho Wa Kukithirisha Swawm Mwezi wa Al-Muharram Na Swiyaam Ya Taasu'aa na 'Aashuraa (9 na 10 Al-Muharram Pamoja Na Masiku Mengineyo)

 

 

Nasiha Na Ukumbusho Wa Swawm  Siku Ya Taasu'aa (9) Na 'Aashuraa (10)

 

 

Fadhila Za Swiyaam Za Fardhi Na Za Sunnah

 

01-Al-Muharram: Mafunzo Katika Miezi Ya Hijri: Ya Kutekeleza Na Ya Kujiepusha

Amali Za Kutenda Na Mambo Ya Kujiepusha Nayo Katika Miezi Mitukufu

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّـهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّـهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿٣٦﴾

Hakika idadi ya miezi mbele ya Allaah ni kumi na mbili katika hukmu ya makadirio ya Allaah, (tangu) siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo, (iko miezi) minne mitukufu. Hivyo ndiyo Dini iliyo nyoofu. Basi msijidhulumu humo nafsi zenu (kwa kufanya maasi), na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita nyote. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa. [At-Tawbah: 36]

 

Na Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth:

 

عن أبي بَكْرَةَ رضي الله عنه عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أنه قَالَ:  إن الزَّمَانَ قَدْ اسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْمَ خَلَقَ اللَّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ السَّنَةُ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ثَلاثٌ مُتَوَالِيَاتٌ ذُو الْقَعْدَةِ وَذُو الْحِجَّةِ وَالْمُحَرَّمُ وَرَجَبُ مُضَرَ الَّذِي بَيْنَ جُمَادَى وَشَعْبَانَ

Imepokelewa kutoka kwa Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mgawano wa zama umerudi katika hali yake ya asili siku Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili; minne miongoni ya hiyo ni mitukufu, mitatu inafuatana pamoja; Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Al-Muharram, mwengine ni Rajab wa (kabila la) Mudhwarr ambao uko baina ya Jumaadaa na Sha'baan))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Fadhila Za Mwezi Wa Al-Muharram

 

1-Swawm (funga) yake ni swawm bora kabisa baada ya Ramadhwaan

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ )) رواه مسلم

Imepokelewa na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Swiyaam (funga)  bora kabisa baada ya Ramadhwaan ni swawm ya mwezi wa Allaah wa Al-Muharram)) [Muslim]

Pia:

 عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : "مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَحَرَّى صِيَامَ يَوْمٍ فَضَّلَهُ عَلَى غَيْرِهِ إِلّا هَذَا الْيَوْمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَهَذَا الشَّهْرَ يَعْنِي شَهْرَ رَمَضَنِان " رواه البخاري

Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhwiya-Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: "Sijapata kumuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akipania kufunga swawm siku yoyote kama siku hii ya siku ya 'Aashuraa na mwezi huu yaani mwezi wa Ramadhwaan" [Al-Bukhaariy]  

 

 

2-Swawm ya 'Ashuraa imependezeshwa hata kwa watoto kuifunga 

 

 عَنِ الرُّبَيِّعِ بِنْتِ مُعَوِّذِ ابْنِ عَفْرَاءَ، قَالَتْ: أَرْسَلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ غَدَاةَ عَاشُورَاءَ إِلَى قُرَى الْأَنْصَارِ، الَّتِي حَوْلَ الْمَدِينَةِ: ((مَنْ كَانَ أَصْبَحَ صَائِمًا، فَلْيُتِمَّ صَوْمَهُ، وَمَنْ كَانَ أَصْبَحَ مُفْطِرًا، فَلْيُتِمَّ بَقِيَّةَ يَوْمِهِ)) فَكُنَّا، بَعْدَ ذَلِكَ نَصُومُهُ، وَنُصَوِّمُ صِبْيَانَنَا... رواه البخاري ومسلم  

Kutoka kwa Ar-Rubay'i bint Mu'awwidh (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma ujumbe Alfajiri ya siku ya 'Ashuraa katika vijiji vya Answaar kwamba: ((Aliyeamka akiwa amefunga swawm bali akamilishe swawm yake, na aliyemka amefuturu amalize siku yake)) [yaani kutokula] Akasema: Tulikuwa tukifunga swawm baada yake na tukiwafungisha watoto wetu...' [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

3-Sababu Ya Kufunga Siku Ya 'Aashuraa  
 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ فَرَأَى الْيَهُودَ تَصُومُ يَوْمَ عَاشُورَاءَ فَقَالَ: ((مَا هَذَا ؟)) قَالُوا : هَذَا يَوْمٌ صَالِحٌ، هَذَا يَوْمٌ نَجَّى اللَّهُ بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنْ عَدُوِّهِمْ فَصَامَهُ مُوسَى، قَالَ: ((فَأَنَا أَحَقُّ بِمُوسَى مِنْكُمْ))  فَصَامَهُ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ

Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alielekea Madiynah akawaona Mayahudi wanafunga swawm siku ya 'Aashuraa, akasema: ((Nini hii?)) (yaani kwa nini mnafunga?) Wakasema: Hii ni siku njema, hii ni siku Allaah Aliyowaokoa wana wa Israaiyl kutokana na adui wao, na Muwsaa alifunga swawm siku hii. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mimi nina haki zaidi juu ya Muwsaa kuliko nyinyi)). Akafunga swawm siku hiyo na akaamrisha ifungwe" [Al-Bukhaariy]    

 

Lakini Nabiy wetu (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamrisha tukhitilafiane na Mayahudi kwa kufunga swawm siku moja kabla yake.

 

روى عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قال : "حِينَ صَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ يَوْمٌ تُعَظِّمُهُ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((فَإِذَا كَانَ الْعَامُ الْمُقْبِلُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ صُمْنَا الْيَوْمَ التَّاسِعَ)) قَالَ فَلَمْ يَأْتِ الْعَامُ الْمُقْبِلُ حَتَّى تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ". رواه مسلم 

Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Alipofunga swawm Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya 'Aashuraa na akaamrisha ifungwe wakasema:  Ee Rasuli wa Allaah!  Hii ni siku wanayoitukuza Mayahudi na Manaswara.  Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ikifika mwakani In shaa Allaah tutafunga swawm siku ya tisa pia)). Akasema (Ibn 'Abbaas) haukufika mwaka uliofuata ila alifariki Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Muslim]

 

Kwa hiyo ni bora kufunga swawm siku ya tisa na kumi (9, 10 Al-Muharram) na kama mtu hakujaaliwa basi afunge swawm siku ya kumi na kumi na moja (10, 11 Al-Muharram), na kama hakujaaliwa basi asikose kufunga siku ya kumi pekee (10 Al-Muharram) ili asikose fadhila zake kabisa.

 

 

4-Bid'ah Katika Siku Ya 'Aashuraa

 

Katika mwezi huu wa Al-Muharram, siku ya 'Aashuraa (tarehe 10 Al-Muharram) baadhi ya watu hufanya maandamano na kuvaa nguo nyeusi wakidai ni nguo za msiba, na huku wakijipiga vifua kwa ngumi na wengine kujikata kwa visu, kujipiga kwa minyororo na damu kuwamwagika, wakidai wanaomboleza kifo cha Al-Husayn (Radhwiya Allaahu 'anhu). ‘Ulamaa wote wa Kiislamu wamepinga na kukemea mno tendo hilo. Hakika hizo ni tabia na mila za Kimajusi za huko Fursi ambayo ni Iran ya sasa.

 

Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

"Bid'ah zinazofanyika katika siku hii ni kuwa baadhi ya watu wameitenga na kuifanya kuwa ni siku ya huzuni kwa kuuliwa Al-Husayn (Radhwiya Allaahu 'anhu). Hivyo watu hulia na kujipiga na hali Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha hayo kwa dalili:

 عَبْد الله ابْن مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَيْسَ مِنَّا مَنْ ضَرَبَ الْخُدُودَ وَشَقَّ الْجُيُوبَ وَدَعَا بِدَعْوَى الْجَاهِلِيَّةِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Si miongoni mwetu anayejipiga mashavu, akapasua mifuko na akaomba maombi ya kijaahiliyyah)). [Al-Bukhaariy]

 

Bali juu ya hayo, wanatukana na kuwalaani Maswahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika siku hiyo."

 

Ibn Rajab amesema:

"Wanayoyafanya Raafidhwah (Mashia) katika siku hii kuwa ni siku ya huzuni kwa ajili ya kuuliwa Al-Husayn (Radhwiya Allaahu 'anhu) ni amali ambazo anazopoteza mtu katika uhai wake akadhani kuwa anafanya amali njema. Wala Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuamrisha kufanya siku za misiba na vifo vya Manabii kuwa ni siku za huzuni, sasa vipi iwe siku ya huzuni kwa wasio Manabii?"

 

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuongoze katika njia iliyonyooka na Atuthibitishe nayo. Aamiyn.

 

 

 

 

Share