Mali Haitomsadia Mtu Kujiokoa Na Jahannam

 

Mali Haitomsadia Mtu Kujiokoa Na Jahannam

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾ 

Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka [Aal-‘Imraan: 90]

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Anasema vitendo vyema vya wale waliokufuru havitapokelewa kwao siku ya Qiyaamah hata kama wataleta dhahabu ya kujaza dunia nzima.

 

Amesema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

   

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لِيَفْتَدُوا بِهِ مِنْ عَذَابِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنْهُمْ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٣٦﴾

Hakika wale waliokufuru, kama watakuwa na yale yote yaliyomo ardhini na mengineyo mfano kama hayo, ili watoe fidia kwayo kuepukana na adhabu ya Siku ya Qiyaamah, hayatokubaliwa kutoka kwao, na watapata adhabu iumizayo. [Al-Maaidah: 36]

 

 

Faida ziada kutoka katika Hadiyth ifuatayo:

 

عن أنس بن مالك عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (( يُقَالُ لِلرَّجُلِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ : أَرَأَيْتَ لَوْ كَانَ لَكَ مَا عَلَى الأرْضِ مِنْ شَيْءٍ ، أَكُنْتَ مُفْتَدِيًا بِهِ ؟ قَالَ: فَيَقُولُ: نَعَمْ . قَالَ: فَيَقُولُ : قَدْ أَرَدْتُ مِنْكَ أَهْوَنَ مِنْ ذَلِكَ، قَدْ أَخَذْتُ  عَلَيْكَ فِي ظَهْرِ أبيك آدَمَ ألا تُشْرِكَ بِي شَيْئًا، فَأَبَيْتَ إِلا أَنْ تُشْرِكَ))  .البخاري، ومسلم.

Imetoka kwa Anas bin Maalik kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kasema: ((Ataambiwa mtu wa motoni siku ya Qiyaamah:  Unaonaje kama ungelikuwa na kitu ardhini je,  ungelifidia nacho? (yaani moto). Akasema: Atasema (huyo mtu): Ndio. Akasema: Atasema: Nilitaka kutoka kwako jepesi zaidi ya hilo. Nimechukua mgongoni mwa baba yako Aadam (ahadi) kwamba usinishirikishe na kitu lakini umekataa ila kufanya shirki))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu kafiri 'Abdullaah Bin Jud'aan ambaye alikuwa mkarimu kwa wageni akisaidia wenye madeni na akilisha masikini:

 

Je, ‘amali zake hizo zitamnufaisha?  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

 

((لاَ, إنه لم يقل يوما من الدهر: رب اغفر لي خطيئتي يوم الدين))

((Hapana, kwani hata siku moja katika maisha hakutaja: Ee Rabb wangu nighufurie  madhambi yangu Siku ya Dini (Qiyaamah)) [Muslim]

 

Faida nyengine katika Hadiyth

 

عن أنس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((يُؤْتَى بِالرَّجُلِ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَقُولُ لَهُ: يَا ابْنَ آدَمَ، كَيْفَ وَجَدْتَ مَنـزلَكَ ؟ فَيَقُولُ: أَيْ رَبِّ، خَيْرُ مَنـزلٍ. فَيَقُولُ: سَلْ وَتَمَنَّ . فَيَقُولُ: مَا أَسْأَلُ وَلا أَتَمَنَّى إِلا أَنْ تَرُدَّنِي إِلَى الدُّنْيَا فَأُقْتَلَ فِي سَبِيلِكَ عَشْرَ مِرَار - لِمَا يَرَى مِنْ فَضْلِ الشَّهَادَةِ. وَيُؤْتَى بِالرَّجُلِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ فَيَقُولُ لَهُ: يَا ابْنَ آدَمَ، كَيْفَ وَجَدْتَ مَنـزلَكَ ؟ فَيَقُولُ: يا رَبِّ شَرُّ مَنـزلٍ. فَيَقُولُ لَهُ: تَفْتَدِي مِني بِطِلاعِ الأرْضِ ذَهَبًا؟ فَيَقُولُ: أَيْ رَبِّ، نَعَمْ. فَيَقُولُ: كَذَبْتَ، قَدْ سَأَلْتُكَ أَقَلَّ مِنْ ذَلِكَ وَأَيْسَرَ فَلَمْ تَفْعَلْ، فيُرَد إلى النَّارِ)) أحمد

 

Imetoka kwa   Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ataletwa mtu katika watu Jannah na ataulizwa: "Ee mwana Aadam! Umeonaje makazi yako? Atasema: "Rabb wangu! Ni makazi bora kabisa." (Allaah Atasema):   "Omba na tamani." Huyo mtu atasema: "Naomba na kutamani tu kuwa unirudishe duniani ili niuliwe mara kumi kwa ajili Yako." kwa sababu ya kuona fadhila za kufa shahidi.  Na ataletwa mtu kutoka watu wa motoni Atasema: "Ee mwana Aadam! Unaonaje makazi yako?" Atasema: "Ni makazi mabaya kabisa Rabbi." Atamuuliza: "Utafidia  nafsi yako kutoka kwangu  kwa ardhi iliyojaa dhahabu?" Atasema: "Ndio Rabbi." Atasema: "Umesema uongo.  Nilikuambia ufanye lililokuwa dogo na jepesi kuliko hilo lakini hukulifanya." Na atarudishwa tena motoni)) [Ahmad, ameisahihisha Al-Albaaniy – Swahiyh Al-Jaami’ (7996), As-Silsilah Asw-Swahiyha (3008)]  

 

 

 

 

Share