Hilaal: Tunaambiwa Wanaofuata Mwezi Wa Kimataifa Wamekosea Na Walipe Swawm, Ni Sawa?

 

Hilaal (Mwandamo Wa Mwezi)

 

Tunaambiwa Wanaofuata Mwezi Wa Kimataifa Wamekosea

Na Walipe Swawm, Je, Ni Sawa?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

SWALI:

 

Napenda kuuliza maswali mawili ambayo yananitatiza katika maelezo tuliyuyapaya kutoka kwa masheikh mbalimbali. kuna masheikh wenye msimamo wa kufunga/ kufungua kwa kufuata muandamo wa mwezi kitaifa wanasema mwaka huu waliofungua kwa kufuata muandamo wa mwezi kimataifa wamekosea kwani hakuna sehemu yeyote duniani mwezi uliondama siku ya alkhamis,kwa hiyo watu waliokula sikukuu siku ya ijuamaa wamekula ramadhani mchana na walipe na hata wakilipa haitokubaliwa, je hii ni sahihi?

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Ni hakika kuwa haya mas-ala tumeyatia u’aswabiyah (kasumba) na ushabiki mpaka tukasahau Uislamu ambao umekuja kuondoa ujahiliya wa kikasumba na kitaifa.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  “Si katika sisi anayeita watu katika utaifa (kasumba n.k.) ” [Abuu Daawuud].

 

Sisi tunasema ipo misimamo miwili mikuu iliyochukuliwa na Wanachuoni wa Kiislamu – msimamo wa kufuata mwandamo wa kitaifa na kimataifa. Hata hivyo msimamo wa mwandamo wa kimataifa ndio wenye dalili za nguvu zaidi lakini hatuwachukulii wenye kufuata mwezi wa kitaifa kuwa funga zao ni batili. Hakika ni kuwa mwenye kujua usawa halisi wa funga na 'Ibaadah nyingine ni Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa) Peke Yake. 

 

Kisha huu msimamo wa kitaifa unakuaje? Kwa mfano, ikiwa mwezi umeonekana Namanga, Kenya na haukuonekana Namanga ya Tanzania au sehemu nyingine yoyote katika Tanzania, je Waislamu wa Tanzania watafunga? Ikiwa kweli watafunga kama inavyofanyika, kweli watakuwa wamefuata mwezi wa kitaifa au kieneo?

 

 

Na  Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share