Akiswali Pekee Swalah Za Jahriyyah (Za Kusomwa Kwa Sauti), Ni Lazima Atoe Sauti?

 

SWALI:

Nashkuru sana kwa kupata nafasi kama hii yakuweza kusoma na kuskiza mawaidha na manufaa mengi kutoka kwa hii website.mungu awajazi kheri na awajaalie muzidi kutupa faida,amin

Swali langu ni kuwa kama twasali swala ya maghrib au ishaa,je nilazima tusome suatul faatiha na sura nyengine kwasauti hata kama naswali pekeyangu?

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Inafahamika kwa kila mmoja wetu kuwa Ibadah ya Swalah inatakiwa tufuate muongozo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hii ni kwa mujibu wa maneno yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

"Swalini kama mulivyoniona nikiswali" (al-Bukhaariy).

Kwa ajili hiyo hata kama Muislamu anaswali peke yake yake Swalah ya kutoa sauti kama Alfajiri, Maghrib au 'Ishaa inafaa atoe sauti. Wanachuoni wanasema kuwa kutoa sauti katika Swalah za sauti ni katika Sunnah iliyokokotezwa (iliyohimizwa) sana hivyo haifai kwa Muislamu kuacha kufuata kwa makusudi.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share