Hilaal: Mwezi Ulionekana Siku Moja Nchi Nyingine Mapema Zaidi Yetu Je, Tulipe Siku Hiyo?

 

Hilaal (Mwandamo Wa Mwezi)

 

Mwezi Ulionekana Siku Moja Nchi Nyingine Mapema Zaidi Yetu

Je, Tulipe Siku Hiyo?

 

 Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

A. aleykum,

Nengependa kupata ufafanuzi wa haya; je wakati tupo mwezi 29 Ramadhani yasemekana baadhi ya maeneo ya Nijeria? Nimeyapata haya kupitia radio na pakatolewa ushahidi wa internet juu ya madai hayo. Ikiwa hivyo itathibitika je tutalazimika kuilipa siku hiyo kwa sie tunaefuata mwezi ma kimataifa?

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

 

Inafahamika misimamo mikuu kuhusu suala la mwandamo wa mwezi ni miwili. Nayo ni kama ifuatayo: 

  • Mwezi wa kimataifa. 
  • Mwezi wa kwetu (kitaifa).

 

Hii miono imegawanyika kwa kiasi kikubwa kutegemea maeneo wanayokaa Waislamu.

Ama wenye kufuata mwezi wa kwetu (kitaifa) mara nyingi hilo halipatikani.

 

Utapata kuwa wapo Waislamu ambao wana muono wa mwezi wa kimataifa lakini kihakika wanafuata mwandamo wa Saudia pekee. Hii inaleta nadharia kuwa msimamo wao sio thabiti kwani mara nyingi zinakuja habari kutoka mataifa wa Waislamu lakini zinakataliwa. Ama kwa hakika wenye msimamo huu wanafaa wafuate mwezi unapothubutu kwa mara ya kwanza kutoka sehemu yoyote ile ye ulimwengu na si mpka tu Saudia wauone au watangaze. Ingawa hata hivyo, Saudia mara nyingi hutokea huwa ndio wa mwanzo kuuona mwezi.

 

Hali ikiwa ni hiyo, ikiwa mtu kweli ana msimamo wa mwandamo wa kimataifa anatakiwa afuate msimamo huo kisawasawa bila kubagua kuonekana na Waislamu kutoka sehemu yoyote ya ulimwengu. Na kwa mfano ikiwa utachelewa kupata habari kama ulivyosikia kuwa Nigeria waliuona mwezi mwanzo kuliko nchi nyingine za Waislamu. Ikiwa hizo ni taarifa za kweli na zenye kuthibitika (maana hatukuweza kuthibitisha hilo), basi unachotakiwa siku hiyo uilipe baada ya Ramadhaan.

 

 

Baada ya kusema hayo, yeyote anayefuata mwandamo wa kimataifa anafaa awe ataulizia habari ya sehemu zote hasa zile ambazo huwa na ada ya kuona mwanzo kama Nigeria, Yemen, Saudia, Kuwait na kadhalika. Kuna baadhi ya nchi huwezi kuzihesabu kama Libya maana wao wanafuata mahesabu yao wenyewe ya mwezi na hivyo taqriban kila mwaka huwa wanatangaza mwezi mapema kuliko nchi nyingine yoyote ile duniani.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share