Vitumbua - 1

Vitumbua  - 1

Vipimo
1 Kikombe cha mchele.
1 Kijiko cha kulia cha unga wa ngano.
3/4-1 Kikombe cha tui la nazi zito.
2 Mayai.
1  Kijiko cha chai cha hamira.
1/2- 3/4 kikombe cha sukari.  
Iliki kiasi upendacho.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Osha na kuroweka mchele ndani ya maji ya baridi masaa manane au siku moja
  2. Mimina vifaa vyote ispokuwa sukari, ndani ya blender na usage mpaka mchele uwe umesagika kabisa.
  3. Mimina sukari ndani ya mchanganyiko na usage tena kidogo tu.
  4. Mimina mchanganyiko ndani ya bakuli na ufinike. Weka bakuli mahali penye joto ili mchanganyiko uuumuke.
  5. Mchanganyiko ukisha umuka, weka karai kwenye moto.
  6. Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia  kila kitumbua.
  7. Mimina mchanganyiko kiasi kwenye karai kulingana na kikarai unachotumia. Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
  8. Panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.

 

 

Share