Vikate Duara Vya Jibini

Vikate Duara Vya Jibini 

 

Vipimo 

 

Unga wa ngano -  4 Magi (vikombe vikubwa vya chai)

 

Maziwa -  1 ½ - 2 Magi

 

Mafuta au siagi -  ¼ Magi

 

Sukari - 1 Kijiko cha supu

 

Hamira -  1 Kijiko cha supu

 

Chumvi -  ¼ Kijiko cha chai

 

Baking powder - 1 Kijiko cha chai

 

Jibini ya malai (cream cheese) - 1 Kikopo au pakiti

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika bakuli, changanya vitu vyote katika vipimo isipikuwa cream cheese.
  2. Kisha ukande kiasi tu kulainisha unga uwe mlaini kama mfano wa unga wa maandazi.
  3. Pakaza siagi katika treya ya kuchomea yenye vishimo.
  4. Halafu fanya viduara na tia ndani yake jibini ya malai kwa kutumia kijiko cha chai, na vifunge viduara vizuri na kuvipanga ndani ya ile treya.
  5. Iwache iimuke (ifure) kisha ipike kwenye oveni moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 – 25, Kisha washa moto wa juu kidogo tu ili iwive na kugeuka rangi.
  6. Toa katika oveni na itakuwa tayari kwa kuliwa.

 

Share