Watoto Wa Chupa (Test Tube) Wana Hukmu Gani Katika Uislaam

 

SWALI:

 

Are test tube babies/ baby implants acceptable (halal) in Islam? Adoption of babies who will then carry the sir name of the non biological father?

 

 


 

JIBU:

 

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo zuri. Ama kuhusu watoto wa test tube (chupa) asli ni kuwa Uislamu haukubali lakini unaukubali tu pindi masharti yaliyowekwa na wanazuoni kutekelezwa.

 

Masharti yenyewe ni kama yafuatayo:

 

i)                   Lazima wanandoa wawe wafunga ndoa ya halali.

ii)                  Iwe mke hawezi kuzaa kwa njia ya kawaida.

iii)                Mbegu za uzazi ni lazima zitoke kwa wanandoa wenyewe.

 

Ama kuhusu adoption (kupanga mtoto) ni jambo ambalo limehimizwa sana na Uislamu hasa wakiwa watoto ni mayatima au watoto wa jamaa au kuwasaidia masikini katika suala hilo. Hakika ni jambo lenye thawabu nyingi sana katika Uislam. Hata hivyo, Uislamu umemkataza mlezi huyo kumbadilisha jina la babake mtoto huyo na kuweka jina lake. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Allaah Aliyetukuka:

'Waiteni kwa ubini wa baba zao, maana huo ndio uadilifu mbele ya Allaah. Na kama hamuwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini na rafiki zenu' (33: 5).

Aayah hii iko wazi kabisa katika kumkataza mlezi kumuita mtoto anayemlea kwa jina lakehata hamjui baba yake.

 

Kwa maelezo zaidi ingia katika kiungo kifuatacho:

 

Uzazi Wa Kupandikiza Wa Chupa (Test Tube) Unafaa?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share