Kutazama Picha Za Uchafu Kwa Ajili Ya Kujitayarisha Na Ndoa Inajuzu?

 

Kutazama Picha Za Uchafu Kwa Ajili Ya Kujitayarisha Na Ndoa Inajuzu?

 

Alhidaaya.com

 

Swali: 

 

Kanijia mtu kisha akaniuliza swali.

 

Anasema Kuwa Yeye Hajawahi kufanya uchafu wa zinaa, na anatarajia kufunga ndoa mwezi wa saba, anaweza kuangalia picha za ex kwa ajili ya kujiandaa, ili asijekupatwa na aibu wakati atakapokuwa ndani na mke wake, kwa sababu hajui hili wala lile kwa upande wa mwanamke, kwa hivyo ndio anauliza swali inafaa? 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

Kuhusu kuangalia picha za uchi au picha chafu zozote kwa sababu yoyote ile haifai katika Uislamu. Hili hata kimantiki haliingii akilini kwani wale ambao utakuwa ukiwaangalia watakuwa katika hali ya uchi ambayo imekatazwa na Uislamu. Picha hizo zinamtia mwanamme ashiki ya bure na hivyo kumkaribisha yeye na zinaa.

 

Jambo ambalo anafaa kufanya ni kupata vitabu vya Kiislamu ambavyo vinaelezea suala hilo kwa muono unaofaa kidini. Pia anaweza kukaa na mashaykh ambao watamfunza kwani mas-ala hayo ya ngono hasa usiku wa kwanza yameelezewa na Uislamu. Na tendo la ndoa limeezewa kinaganaga katika Qur-aani na Sunnah, kwa nini sisi tutafute njia nyingine mbaya?

 

Mwambie ndugu yetu asitie wasiwasi kwani hilo si jambo zito bali ni jambo la kawaida kabisa na ni suala la kimaumbile na unapofika wakati ataliona kuwa ni jepesi na rahisi kufahamika. Ikiwa hukupata vitabu hivyo wala Shaykh ambaye anaweza kukupatia muongozo kuhusu hilo basi inafaa ukae na mtu uliye karibu naye ambaye tayari ameoa naye atakupa nasaha na maelezo yanayofaa.

 

Hata hivyo, sisi katika ALHIDAAYA tuna kitabu kizuri sana kwa mafunzo ya ndoa yote pamoja na jinsi ya kuishi na mkeo. Ingia hapa chini usome:

 

Zawadi kwa Wanandoa

 

Hiki kingine cha ziada kwa faida:

 

Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika (Aadabu Az-Zafaaf Fiy As-Sunnat Al-Mutwahharah)

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share