Kampa Dada Yake Kama Zawadi Aishi Naye Kinyumba Nini Hukmu Yake?
SW
Assalam alaykoum,
Tafadhali naomba ufafanuzi na jawabu kwa suala langu hili:
Kuna mwanamume mmoja asiyejiweza (masikini) aliyempa dada yake kwa mwanamume mwengine, aishi nae kinyumba
Na huyu mwanamume aliyepewa huyu dada amesema ni halal yake kwani imeruhusiwa kwa Qur'an na
Wameishi pamoja zaidi ya mwaka sasa, huyu bibi ni mja mzito na atajifungua wakati wowote. Swali langu ni jee hii hadiya ya kupeana mwanamke inajuzu kwa dini yetu? Jee ni haram au ni halal?
Shukran na jazzakumu llahu khairan.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ‘hiba’
- Kuwepo kwa walii wa mke.
- Kukubali kuolewa mwanamke mwenyewe.
- Kuwepo kwa mashahidi wawili waadilifu.
- Mwanamme kutoa mahari waliyosikilizana na atakayekuwa mkewe.
- Mwanamme naye kuridhia kwa ndoa sio kuishi kinyumba.
Allaah Aliyetukuka Anasema yafuatayo kuhusu kuwaweka wanawake kinyumba:
“Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapowapa mahari
Ndugu hana haki kabisa hata akiwa masikini kiasi gani kumtoa dada yake ili awekwe na mwanamme mwengine kinyumba kwani
Ama kuhusu maa malakat aymaanukum (sio ‘aymaanikum’
Kuhusu mfano uliotolewa wa ‘Umar na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma) hauingii kabisa kwani ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuoa binti wa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa akiitwa Ummu Kulthuum na wala hakupewa zawadi.
Kwa ufupi, ni kuwa hao wenye kukaa kinyumba wanazini na hiyo mimba si ya halali kabisa. Wanapaswa waachane haraka
Kwa ufupi ni kuwa kufanya hivyo ni haramu.
Na Allaah Anajua zaidi