Zingatio: Ni Ajabu

 

Zingatio: Ni Ajabu

 

 Naaswir Haamid

 

 Alhidaaya.com

 

 

Ni mengi ambayo tumeelezwa ndani ya Qur-aan na Sunnah kwa lengo la kupata uongofu. Lakini ni wachache mno wanoelewa hayo. Hata kwa wanaosadiki ukweli huu, kwa namna fulani wanashindwa kuyatekeleza kwa matendo.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tumewaweka kando na tunawajua kuwataja kwa nyakati za dhiki au kejeli. Utamuona Muislamu ni mwenye kumsujudia mno Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) pindi shughuli zake za rizki zinapoharibika. Zinapotengenea, huacha ibada hizi kana kwamba hakuwahi kukutwa na mashaka hayo. Wengine wanasubiri hadi ugonjwa uwagongee mlango au Malakul-Mawt awatembelee ndio waanze kuomba msaada kwa kuzitaja kulla aina ya tasbiyh. Si hayo tu, bali tunashuhudia utovu wa nidhamu kwa Rabb Mlezi kwenye miziki.

 

Sauti zapandishwa kumtaja Allaah,

Mwanamke aitoa sauti chini ya mvungu;

Huku ala za muziki zikifunguliwa pingu,

Wana hao wa Shaytwaan wanalipika jungu;

Linalojazwa dhambi na laana za Allaah,

Wasahau kabisa kuwa wamkasirisha Rabb wa Mbingu.

 

Tutambuwe ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameruhusu matumizi ya mashairi katika arusi na siku ya ‘Iyd kwa masharti kwamba mashairi hayo yasiwe na kejeli, matusi, wala kashfa, na kusiwemo ndani yake ala za taarabu mfano gita na firimbi[i]. Sasa kwa wale Waislamu wakike na wakiume wanaoimba taarabu kwa kutumia majina ya Allaah na sifa Zake, wameipata wapi ruhusa hiyo?

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hakutuumba bure bure tu. Tumeletwa hapa kumuabudu Yeye tu, Rabb wa ‘Arshi yenye hadhi kubwa kabisa. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ ﴿١١٥﴾فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ ﴿١١٦﴾

Je, mlidhania kwamba Sisi Tulikuumbeni bila kusudio mcheze tu na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa?Je, mlidhania kwamba Sisi Tulikuumbeni bila kusudio mcheze tu na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa? [Al-Muuminuwn:115-116]

 

Alichokuja nacho Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni lazima tukifuate, na yeye ni Mwonyaji. Dalili zilizo nyingi kuhusu Qiyaamah zimeshatokea. Ni lazima tuachane na matamanio ya nafsi kwa kuichezea shere hukumu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

أَفَمِنْ هَـٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ ﴿٥٩﴾وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ ﴿٦٠﴾وَأَنتُمْ سَامِدُونَ ﴿٦١﴾فَاسْجُدُوا لِلَّـهِ وَاعْبُدُوا ۩﴿٦٢﴾

Je, mnastaajabu kwa Al-Hadiyth hii (ya Qur-aan)?Na mnacheka na wala hamlii?Na hali nyinyi mnaghafilika, mnadharau na kushughulika na anasa? Basi msujudieni Allaah na mwabuduni Yeye. [An-Najm: 59-62]

 

Tunafupisha hapa kwa kueleza: Ni wajibu wa Waislamu kurejea katika hukumu tukufu za Shariah ya Kiislamu.

 

[i] Uswuulul al-Mu’asharata az-Zawjiyaah, Qaadhi ash-Shaykh Muhammad Ahmad Kan’aniy, uk. 52.

 

Share