Pilau Ya Bilingani Na Kuku

Pilau Ya Bilingani Na Kuku

 

Vipimo

 

Mchele wa basmati - 3 vikombe

Kuku - ½

Bilingani - 2 ya kiasi

Viazi - 4

Vitunguu - 2

Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 2

Chumvi - kiasi

Garama masala (mchanganyiko wa bizari) - 1 kijiko cha chai

Hiliki ya unga - ¼ kijiko cha chai

Mafuta ya kupikia wali - ¼ kikombe

Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

  1. Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
  2. Kata kuku vipande upendavyo safisha
  3. Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala). 
  4. Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
  5. Menya na kata viazi kaanga weka kando.
  6. Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando.
  7. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo.
  8. Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa.
  9. Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive.
  10. Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.

 

 

                                                                

Share