Mchuzi Wa Mumunye (Zucchini) Na Viazi

Mchuzi Wa Mumunye (Zucchini) Na Viazi 

 

Vipimo 

Zucchini -  3 

Viazi - 2 

Kitunguu - 1 

Nyanya - 2 

Nyanya kopo - 2 vijiko vya supu 

Pilipili manga - kidogo 

Pilipili mbichi -  2 

Kidonge cha supu (stock) - 1 

Ndimu -  Nusu  

Mafuta - 2 vijiko vya supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata mamumunya (zucchini) vipande vya duara,  viazi vipande vya kiasi, nyanya, na kata kitunguu vidogo vidogo (chopped).
  2. Tia mafuta katika sufuria, kaanga viitunguu hadi viigeuge rangi kidogo tu.
  3. Tia nyanya endelea kukaanga hadi ziwive, tia nyanya kopo
  4. Katia pilipili mbichi, tia pilipilimanga, chumvi .
  5. Tia maji kiasi, viazi, tia kidonge cha supu, funika weka moto mdogo acha hadi karibu viazi kuwiva, tia mamumunya.
  6. Bakisha kidogo motoni uwivishe mamumunya kidogo tu .
  7. Kamulia ndimu na tayari kuliwa kwa wali au mikate yoyote upendayo.

 

 

Share