Mume Kaniingilia Wakati wa Eda – Hatimizi Sheria Za Kunihudumia??

SWALI:

 

Assalam aleykum ndugu wa alhidaaya,

 

Nimefuata ushauri na kupata talaka yangu kutoka kwa kadhi na sasa nipo kwenye eda lakini jana kaja mtalaka wangu na kudai hakubaliani na talaka kisha kaniingilia kwa kunilazimisha je nifanyeje? Kwani nilidai talaka kutokana na mambo mengi ambayo huyu mwanaume hayatimizi karibu sheri zote nda ndoa hakuzifuata na sasa sijielewi naomba msaada kutoka kwenu ndugu zangu waislam na Mwenyeezi Mungu Mola wa ulimwengu wote atawapa kheri kwa kutusaidia amen.

 

 

 


JIBU:

 

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu eda na kuingiliwa na mumeo katika wakati huo. Tunakutakia kila la kheri baada ya hayo yaliyokukumba ambayo si mazuri. Kwa kuwa tayari ulikwenda kwa Qaadhi na kupata talaka itabidi urudi kwa Qaadhi ili umuelezee kwani kitendo alichofanya mtalaka wako si katika maadili ya Kiislamu. Na bora vufuate utaratibu huo kuliko kuja kwetu kwanza. Linalotokea lolote rudi kwa Qaadhi la hilo litakuwa sahali kwako wewe hasa.

 

 

Itabidi ikirudi kwa Qaadhi baada ya kumueleza, awe ni mwenye kumsisitizia mtalaka wako asiwe ni mwenye kuja kwako ila aweko yeye asikilize mashtaka na labda ufanye hapo unapoishi usiwe ni mwenye kukaa peke yako ili usikumbane na hayo kwa mara nyengine tena.

 

 

Tunakuombea kila la kheri.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share