Vitumbua - 2

Vitumbua - 2

   

Vipimo

 

Mchele - 2 mugs

 

Tui la nazi - 2 mugs

 

Yai -  1 kubwa

 

Sukari - ½ mug

 

Hiliki - ½ kijiko cha chai

 

Hamira - ½ kijiko cha chai

 

Unga wa ngano -  2 vijiko vya chakula

 

Samli ya kupikia  (au mafuta) - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Osha na roweka mchele kiasi masaa kuanzia mawili au zaidi.
  2. Saga mchele na tui kwenye mashine ya kusagia (blender) mpaka uwe laini usiwe na chenga.
  3. Tia hiliki, hamira na unga wa ngano saga tena mpaka uchanganyike.
  4. Mimina kwenye bakuli na uache uumuke kiasi.
  5. Ukisha kuumuka changanya sukari na yai
  6. Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia  kila kitumbua.
  7. Mimina mchanganyiko kiasi kwenye kikarai maalumu cha kuchomea vitumbua.
  8. Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
  9. Panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.

 

 

Share