Chapati Za Hamira Na Ufuta Za Kuoka (Baked)

Chapati Za Hamira Na Ufuta Za Kuoka (Baked)

 

   

Vipimo

Unga - 4 Mugs

Maziwa - 2 Mugs Kasorobo

Chumvi - kiasi

Baking Powder - 1 kijiko cha chai

Hamira - 1 kijiko cha chai

Unga Kama mlaini shikia na mafuta

Yai -  1

Ufuta -  kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya pamoja unga, chumvi, hamira, baking powder na maziwa. Uchanganye unga na ukande uwe mlaini vizuri.
  2. Fanya madonge kama 8 kwa hicho kipimo cha  unga.
  3. Sukuma kila donge na upake samli na ukunje kama chapatti.
  4. Ukisha maliza sukuma daura, isiwe kubwa kama chapati ina kuwa ndogo na upange kwenye tray ya kuchomea kwenye oven.
  5. Iwache mpaka ikisha umuka, pakaza mayai na nyunyiza ufuta kwa juu.
  6. Choma (Bake) kwenye oven kwa moto wa chini, halafu washa moto wa juu iwe brown.
  7. Ukisha kuutoa pakaza mafuta kidogo kwa juu kwa kutumia brush.
  8. Tayari kwa kuliwa  na chai au mchuzi au kitu chochote.

 

Share