Bajia Za Bilingani, Viazi Na Njegere
Bajia Za Bilingani, Viazi Na Njegere

Vipimo
Bilingani - 1
Viazi - 2
Njegere za kijani (green peas) - 1 kikombe
Pilipili mbichi - 1
Bizari ya pilau iliyosagwa (cumin powder) - ½ kijiko
Chumvi - kiasi
Unga wa dengu - 1 kikombe
Maji - kiasi
Mafuta ya kukaangia katika karai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katakata bilingani bila ya kumenya weka kando.
 - Menya viazi, katakata vipande virefu virefu kama vya chipsi (French fries)
 - Chemsha njegere hadi ziwive epua weka kando.
 - Katakata pilipili mbichi ndogo ndogo sana
 - Changanya vitu vyote na bizari na chumvi.
 - Changanya unga wa dengu na maji kiasi kidogo uwe mwepesi.
 - Teka kidogo mchanganyiko, chovya katika unga wa dengu kisha kaanga katika mafuta ya moto.
 - Epua, chuja mafuta, zikiwa tayari kuliwa kwa chatine ya mtindi na ukwaju na zilioko katika viungo vifuatavyo:
 
Sosi Ya Ukwaju
    
    