Matapishi: Amefunga Hadi Karibu Na Magharibi Kisha Akatapika, Je, Swawm Yake Imesihi?

SWALI:

Assalaam alykum

swali langu ni hili kama umefunga mpaka karibu ya maghrib umetapika itakuwa umefungua au ukamilishe na saumu?

 

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kutapika bila ya kujilazimisha mwenyewe mtu hakubatilishi Swawm. Ni vizuri mtu kuhakikisha pia kuwa matapishi hayarudi tumboni kwa maana hurudi kuyameza baada kutapika huko bila kukusudia.

 

Lakini ikiwa umetapika kwa kujisababishia mwenyewe ima kwa kupiga mswaki hadi ndani kabisa ya koo na hali unajua kuwa itasababisha wewe kutapika, au kujipelekea katika jambo lolote la kutapisha, basi Swawm yako itakuwa imebatilika hata ikiwa ni dakika chache tu kabla ya Magharibi na itaibidi siku hiyo uilipe.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share