Kutoa Damu Kunavunja Swawm?

Kutoa Damu Kunavunja Swawm?

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

asalam alaykum,

suali langu ni hili jee kama mtu amefunga na akaenda hospital akatolewa damu ktk mkono wake kidogo ktk vichupa kama sita kwa ajili ya uchunguzi wa maradhi mbalimbali  funga ya mtu huyu itakuwa inasihii au asifunge kwa siku ilee?

Jazaka llahulkheir

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 atika kila hali msingi wa hilo utatokana na Hadiyth iliyopokewa na Al-Bukhaariy ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliumika akiwa amefunga naye hakufungua.

 

Kwa Hadiyth hii Wanachuoni wamesema ikiwa kutoa damu kule kutamdhoofisha Muislamu na kumtia taabuni basi ni afadhali afungue lakini ikiwa anaona ni sawasawa wala hana shida yoyote basi anaweza kuendelea kufunga na Swawm yake itakuwa inasihi.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share