Niliposukutua Maji Yalishuka Kooni Bila Ya Kukusidia Kuyameza Je, Swawm Yangu Imeharibika?

 

SWALI:

 

asalam aleikum ndugu zangu wa islam nafuraha sana kukuwauliza swali

namukaweza kunijibu mungu awajeze kheri nafanaka.swali langu nihili nilikua nimefunga nikawa namafua nakifua kidogo wakati nimeenda kutawadha wakati wakuskutua mdomo nikaskia kwenye koo kama maji yameshuka na mimi nimeskutua nikatema pale pale naskia kwenye koo kama kitu kimeshuka na sikujua ni mafua ama yalikua yako kwa kooni yakishukha kooni derect ama ni mafua.nakama nimafua yashuka derect kwenye koo na hali nimefunga jee hio zaumu yangu itakubalika na kama nimaji pengine yameshuka kooni kidogo saumu yangu iko ama niilipe.nawatakia kila lagheri na saum makbul inshallah maasalm

 

 


 

 

JIBU

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

  
 Swawm yako haijaharibika na ni sahihi, kwani hukumeza maji kwa kukusudia. Na ambaye amekula au kunywa bila kukusudia, basi Swawm yake ni sahihi. Lakini mtu anapaswa kuwa makini na haswa anapotawadha anatakiwa asisukue au kuvuta maji puani kwa nguvu ili yasije kuingia ndani ya mwili.
 
Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share