Chapati Za Nyama

Chapati Za Nyama 

  

Vipimo  

Unga -  1 ½ vikombe vya chai

 

Mafuta -    ¼ kikombe cha chai

 

Chumvi -   ½ kijiko cha chai

 

Maji -  1 kikombe cha chai 

 

Mafuta -   ½ kikombe cha chai  

 

Mayai-  6 mayai 

 

Manda nyembamba za mraba (Spring roll pastries sheet) -  6 

 

Nyama ya kusaga  - ½ kilo 

 

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi -  1 kijiko cha supu

 

Kotmiri iliyokatwakatwa - ½ kikombe

 

Chumvi -  kiasi 

 

Pilipili manga -    ½ kijiko cha chai 

 

Pilipili mbichi - kiasi (ukipenda)

 

Bizari ya pilau ya unga -  ½ kijiko cha chai. 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika     

  1. Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike   
  2. Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1.
  3. Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu kama nyama ya sambusa , wacha ipoe.
  4. Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba .
  5. Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike kama inavyoonyeshwa kwenye picha.  
  6. Choma kama unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi. 
  7. Weka kwenye sahani tayari kuliwa.

 

Share