Mboga Ya Bok Choy Na Viazi

Mboga Ya Bok Choy Na Viazi

 

Vipimo 

Viazi - 6 Vikubwa

Kitunguu maji - 1 Kikubwa

Bok choy -  6 Vifurushi (bunches) vidogo

Pilipili masala -  Kiasi utakachopenda

Ndimu - 1

Chumvi -  Kiasi upendacho

Mafuta ya kukaangia - 2 vijiko vya supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika.  

  1. Menya viazi na kitunguu maji.
  2. Katakata viazi kama kwenye picha.
  3. Katakata vitunguu vidogo (dice).
  4. Kata vipande vya mwisho vya mboga ya bok choy na uvioshe vizuri uviweke kando. Utatumia hivi kupambia tu.
  5. Osha mboga vizuri pia na uweke kando.
  6. Weka kikaango (frying pan) kwenye moto, mimina mafuta. Yakipata moto mimina viazi, chumvi, na pilipili masala. Kaanga viazi mpaka vianze kuiva kisha mimina vitunguu maj. Viache viazi mpaka vianze kuwa vikavu.
  7. Mimina mboga ya bok choy ndani ya viazi na ukamulie ndimu. Pika kidogo tu kiasi mboga ilegee, kama dakika 3 hivi.
  8. Mimina mboga kwenye bakuli la kupakulia na upambe na vile vipande vya bok choy ulivyokata. Tayari kwa kuliwa na wali au mikate yoyote upendayo.  
Share