Daal (Dengu) Za Nazi Na Viazi

Daal (Dengu)  Za Nazi Na Viazi

      

Vipimo: 

Dengu zilopasuliwa - 2 vikombe

Viazi -  3

Kitunguu - 1

Nyanya - 1

Pilipili mbichi na thomu iliyosagwa  - 1 kijiko cha chai

Methi (uwatu) uliosagwa -   1/2 kijiko cha chai

Majani ya mchuzi (curry leaves) -  kiasi 5

Haldi (bizari ya manjano) -  1/2 kijiko cha chai

Kotmiri iliyokatwa katwa -  1 Msongo (bunch)

Ndimu -  1

Chumvi - kiasi

Tui la nazi - 1 kikombe

Mafuta -  3 vijiko vya supu   

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Roweka dengu kwa muda wa masaa, kisha zichemshe ziwive. Maji tia kiasi tu ili zibakie dengu na supu kidogo tu. 
  2. Karibu na kuiva tia viazi vilivyomenywa na kukatwakatwa vidogo vidogo.
  3. Katakata kitunguu na nyanya, weka kando. 
  4. Weka mafuta katika sufuria ya kiasi, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi. 
  5. Tia majani ya mchuzi kaanga kidogo, tia methi (uwatu), kisha tia thomu na pilipili, nyanya na bizari ya manjano. 
  6. Mimina dengu na viazi vyake kisha tia ndimu, chumvi.
  7. Tia tui la nazi na uache kidogo ichemke, 
  8. Tia kotmiri iliyokatwakatwa ikiwa tayari.

 

 

 

Share