Nguzo Za Fardhi Za Kiislaamu Zimefaridhiwa Lini?

 

Nguzo Za Fardhi Za Kiislaam Zimefaridhiwa Lini?

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Naomba kujua tarehe za kufaradhishwa kwa nguzo tano za Kiislam.

 

Nawatakia kila la kheri

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Nguzo Za Kiislamu zimefaridhiwa kama ifuatavyo:

 

1-Shahaadah – mwaka wa kwanza baada ya kupatiwa Unabiy wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

2-Swalaah – miezi 12 hadi 16 kabla ya Hijrah pale Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alipopelekwa safari ya Israa na Mi’raaj.

 

3-Swawm – mwaka wa pili mwezi wa Sha‘baan baada ya Hijrah.

 

4-Zakaah – mwaka wa pili mwezi wa Sha‘baan baada ya Hijrah.

 

5-Hajj – mwaka wa sita baada ya Hijrah.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share