Mchanganyiko Wa Mboga Za Mvuke (Steam)

Mchanganyiko Wa Mboga Za Mvuke (Steam)

Vipimo

Viazi -  2 

Karoti -  2 

Koliflawa (cauliflower) - ½ 

Brokoli - 3 misongo (bunch) 

Pilipili mboga ya kijani - 1  

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa -1 kijiko cha chai

Pilipili manga iliyosagwa - 1 kijiko cha chai 

*Kidonge cha supu (stock) - 1  

Chumvi - kiasi 

Mafuta ya zaytuni (olive oil) - 3 vijiko vya supu 

Maji - ½ kikombe cha chai 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Menya viazi katakata vipande vya mchemraba (cubes)
  2. Katakata karoti vipande vya duara
  3. Katakata pilipili mboga vipande vya kiasi kiasi
  4. Chambua koliflawa na brokoli
  5. Changanya vitu vyote kwenye sufuria pamoja funika kisha weka katika jiko kwa moto mdogo mdogo.
  6. Ikishawiva kidogo tu ipua mimina kwenye bakuli tayari kuliwa na mkate au wali.

* kidonge cha supu ikiwa ni chicken stock au beef stock.

 

 

Share