Khalyat An-Nahl (Mzinga Wa Nyuki)-2

Khalyat An-Nahl (Mzinga Wa Nyuki) -2

 

Vipimo

Unga - 4 Magi (vikombe vya chai)

Maziwa ya maji - 1 ½ au 2 Magi

Sukari - 1 Kijiko cha supu

Mafuta - Robo Magi

Hamira - 1 Kijiko cha supu

Chumvi - robo kijiko cha chai

Cheese ya Cream - 1 Kikopo au Pakti  

Baking powder - 1 Kijiko cha chai

 

Shira

Sukari - Vikombe 2

Maji - Kikombe 1 ½  

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya vitu vyote hivyo isipokuwa cream cheese.
  2. Kanda kidogo tu kulainisha unga uwe mlaini kama mfano unga  wa maandazi. 
  3. Pakaza siagi katika sinia ya round utakayopikia 
  4. Fanya viduara vidogo vidogo na tia ndani yake cheese ya cream kwa kutumia kijiko cha chai, na vifunge viduwara vizuri na kuvipanga katika sinia  bila ya kuwacha nafasi.
  5. Iwache iumike kisha paka maziwa juu yake kwa brashi kabla ya kuchoma ili kufanya ing’are.
  6. Ipikie katika oven moto wa chini kwanza katika 350˚C, kwa muda wa baina dakika  20  na 25 .  Kisha washa moto wa juu kidogo tu uwive kwa juu.
  7. Toa katika oven na mwagia shira kama ifuatavyo.

    Kama ni shira iliyopowa basi mwagia juu ya mkate uliomoto

   Kama ni shira imoto basi subiri mkate upowe.  Yaani mojawapo iwe moto au baridi.

 

 

Share