Umri Gani Huhesabika Kuwa Ni Mtoto Yatima?

 

Umri Gani Huhesabika Kuwa Ni Mtoto Yatima?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam aleykum warahmatullah wabarakatuh,

 

Shukrani nyingi kwenu kwa kutupa urahisi katika kujua masuala ya dini Allah s.w awape kheir ameen.

 

swali langu ni.... je mtoto aliefiwa na baba au mama kabla ya miaka 18 ni yatima na akipita hiyo miaka na akawa na miaka 25 atakuwa si yatima tena yaani mtoto yatima ni yule mwenye umri chini ya miaka 18????

 

Asanteni.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Ifahamike kuwa yatima katika Uislamu ni yule aliyefiliwa na baba, kwani aliyefiliwa na mama haitwi yatima kabisa. Aliyefiliwa na wazazi wote wawili ni yatima zaidi kuliko aliyefiliwa na baba peke yake.

 

 

Ama umri wa mwanadamu kuitwa yatima ni kabla ya kubaleghe. Akisha baleghe basi anakuwa si yatima tena. Umri wa kubaleghe inategemea mazingira, jinsia, nchi na kabila pia. Ama kwa wasichana wanaweza kubaleghe kuanzia umri wa miaka tisa na mvulana baada ya umri huo, sana sana kuanzia 15.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share