Damu Inayotoka Akiwa Mja Mzito Ni Kama Ya Hedhi Je Aswali?

 

 

 

Damu Inayotoka Akiwa Mja Mzito Ni Kama Ya Hedhi Je Aswali?

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Swali:

 

Asalamu Alaykum: Mimi ndugu yenu muislam nina suali langu linanipa utata naomba ufafanuzi kutoka kwenu. Suali langu ni hili:-

Hivi mtu akiwa mja mzito akawa anablid mara kwa mara na damu inatoa harufu kama ya hedhi jee anaruhusika kuswali? Naomba kujibiwa.
Ahsante.

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Damu inayomtoka mwanamke anapokuwa mja mzito inaweza kuwa ni damu ya hedhi au damu ya kawaida au inaweza kuwa ni damu ya nifaas ikiwa ni karibu na kuzaa.

 

 

Kutokana na ulivyoeleza kuwa unapata damu na inatoa harufu kama ya hedhi basi bila shaka hiyo itakuwa ni hedhi, kwani ‘Ulamaa wamekubaliana kuwa damu huwa damu ya hedhi ikiwa itakuwa na sifa za damu ya hedhi. Hivyo itabidi uache kuswali na kufunga.

 

Rai ya kwamba mwanamke mjamzito anaweza kupata hedhi ni rai ya madhehebu ya Imaam Shaafi'iy ambayo imesimuliwa kutoka Imaam Ahmad. Na vile vile imewafikiwa na Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah,  lakini ni jambo la nadra sana kwa mwanamke kupata hedhi katika hali hiyo. [Al-Ikhtiyaaraat ukurasa 59]  

 

Rai ya Imaam Ibn 'Uthaymiyn ni kwamba, damu huwa ya hedhi ikiwa itakuwa na sifa za damu ya hedhi na hutokea wakati ule anaoutarajia mwanamke kama kawaida yake. [Fataawa Muhammad ibn Ibraahiym 2/97]   

 

Na huwa ni damu ya kawaida ikiwa haina sifa za damu ya hedhi au damu ya nifaas, yaani rangi yake huwa nyekundu na hii huwa ni  'istihaadhwah' (Damu ya hedhi itokayo muda au siku zisizotarajiwa). Na hii ndio inayoitwa 'An-naziyf' (lit. haemorrhage)  

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share